Monday, 9 December 2013

MAAJABU YA MUNGU: NYAMA ILIYOKUWA INAPIKWA YAJITOKEZA JINA LA ALLAH الله, SUFURIA YOTE YAUNGUA

Tukio la ajabu na lisilo katika ada ya kibinadamu limetokea jumamosi iliyopita maeneo ya kijitonyama mtaa wa bwawani jijini Dar es salaam. Tukio hilo lenye mazingatio kwa wenye akili ni pale nyama iliyokuwa inachemshwa kwa ajili ya kitoweo kujitokeza jina la mwenyezi mungu الله.

Akielezea tukio hilo Nia zakaria ambaye ndiye aliyekuwa wa kwanza kugundua anasema walienda kununua nyama kwa ajili kitoweo cha siku hiyo. Walipofika nyumbani waliiandaa kama kawaida kwa ajili ya kuipika.

Wakati inachemka jikoni wao walikuwa sebuleni wakiendelea na mambo mengine. Baadae wakasikia harufu ya kuungua kwa nyama ndipo alipokwenda haraka jikoni kunusuru nyama isiendelee kuungua.

Ajabu alikuta sufuria yote imeungua lakini hakuna kipande chochote cha nyama kilichokuwa kimeungua hata kidogo.
katika kuikagua zaidi nyama hiyo ndipo alipoona jina la Allah الله katika moja ya vipande vya nyama hiyo.

Ajabu nyingine ni pale walipoamua kupiga picha kipande cha nyama hiyo, ni kwamba kila walipopiga ilikuwa ikitokea mchoro wa jina la Allah الله kama mchoro wa moto.

0 comments