Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imetangaza kusimamisha zoezi la
uokoaji wa abiria na mizigo kufuatika boti ya Kilimanjaro ll kupigwa na
dhoruba na kusababisha watu kadhaa na mizigo kutumbukia majini.
Boti hiyo ilipatwa na mkasa huo Jumapili katika mkondo wa Nungwi wakati ikitoka Pemba kwenda unguja.
Baada ya tukio hilo Serikali iliendesha zoezi la uokoaji na miili ya
watu sita iliopolewa na wengine watatu wakiokolewa wakiwa hai.
Hata hivyo, juzi jioni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,
Mohamed Aboud Mohamed, alitoa taarifa ya kusitisha zoezi hilo na
kuwataka wakuu wa wilaya, mikoa, masheha na wananchi kutoa taarifa
watakapoona maiti.
Wakati zoezi hilo likisimamishwa, watu wanane hawakuwa wameonekana kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA), Abdi Omar Maalim.
CHANZO: NIPASHE
0 comments