Atletico Madrid leo wameungana na wapinzani wao Real Madrid katika fainali ya ligi ya mabingwa wa Ulaya baada ya leo kuifumua Chelse goli 3-1 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Starmford Bridge jijini Lomdon.
Jana Real Madrid waliwasambaratisha Bayern munich kwa kuwachapa goli 4-0 na kupelekea matokeo ya jumla kusomeka kwa Real Madrid 5 wakati Bayer Munich wakiwa 0.
Kwisha kazi; Mfungaji wa bao la tatu la Atletico Madrid, Arda Turan akishangilia |
Katika mchezo wa leo Chelsea walikuwa wa mwanzo kupata goli kupiyia kwa Fernando Torres katika dakika ya 36 akitumia vyema pasi ya Azpilicueta baada ya kazi nzuri ya Willian.
Atretico Madrid walisawazisha goli hilo ikiwa imebakia dakika moja kwenda mapumziko kupitia kwa Adrian Lopez akatumia vyema pasi ya Juan Fran.
0 comments