Saturday, 17 May 2014

KUTOKA FB: KWA MAJIBU HAYA SERIKALI TATU WAJIBU

Bajeti ya kikosi cha zima moto imeorodhesha mikoa ya Tanzania Bara pekee. Mbunge kutoka Zanzibar kasimama na kuhoji..."mbona sioni hata mkoa mmoja wa Zanzibar?" Waziri kamjibu ki-mkato tu, "zimamoto sio suala la kimuungano"!

Hapo ndipo hoja ya serikali tatu inapata mashiko. Linapojadiliwa suala ambalo Zanzibar haihusiki, wabunge wa Zanzibar wasije. Kwa maana rahisi ni kwamba, liwepo bunge ambalo litajadili masuala ya Tanzania Bara peke yake kama ilivyo Baraza la Mapinduzi linavyojadili masuala ya Zanzibar pekee(hata kauli ya Werema jana inaonekana ilillenga kitu hicho hicho). Halafu ndio liwepo bunge litakalojadili masuala yenye maslahi ya Bara na Visiwani...ndilo bunge la Muungano. Ikifikia hapo ndipo utapata serikali itakayokuwa inatekeleza maagizo ya bunge la Tanzania Bara...ndio serikali ya tatu hiyo! NAWAZA KWA SAUTI

0 comments