Saturday, 17 May 2014

MAMA MARIA NYERERE AWAKEMEA WASIASA

By    
Mke wa hayati baba wa taifa mama Maria Nyerere ameutaka uongozi uliopo madarakani kutafakari kwa umakini kauli zinazotolewa sasa na baadhi ya viongozi kuhusu utendaji kazi wa waasisi wa taifa akiwemo Mwl. Julius Nyerere

Mama Maria ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam wakati wa mazungumzo na Jumuiko la Vijana Wazalendo na Wapenda Amani waliofika katika makazi yake Msasani kumfariji kwa kashfa ambazo zimetolewa dhidi ya Mwl. Nyerere.

Kabla ya kutoa kauli hiyo, Maria Nyerere anapokea ujumbe wa kundi linalojiita Jumuiko la Vijana Wazalendo na Wapenda Amani waliowakilisha ujumbe wa kulaani kile kinachoitwa matusi na kashfa dhidi ya Hayati Baba wa taifa.

Baada ya ujumbe huo, ndipo mjane huyu naye anatoa kauli yake kuhusu yale ambayo amekuwa akiyasikia na kuyaona yakisemwa bungeni juu ya mumewe

Jumuiko la Vijana Wazalendo na Wapenda Amani linaundwa na vijana wa Chama cha mapinduzi UVCCM pamoja na vijana wengine wasiokuwa wafuasi wa vyama vya siasa. Na hapa wanaitafakari kauli ya Mama Maria

Mijadala iliyojitokeza wakati wa kuchangia juu ya muundo wa serikali na muungano uliopo ndiyo kiini cha malalamiko ya Jumuiko la Vijana Wazalendo na Wapenda Amani ambao wanataka hatua za haraka zichukuliwe ili kulinda heshima za waasisi wa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar
Mwis

0 comments