Monday, 21 July 2014

STEVEN GERRARD ATUNDIKA DARUGA KIMATAIFA

http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/9/99/SGerrard.JPG/220px-SGerrard.JPG
Nahodha wa timu ya taifa ya England Steven Gerrard mwenye umri wa miaka 34 ametangaza kustaafu soka la la kimataifa hii leo, ikiwa baada ya kushudia timu yake ya Taifa ikishindwa kufanya vyema karika kombe la dunia mwaka huu lililo malizika kwa Ujerumani kuwa bingwa.
.
 Akizungumza kwenye tovuti ya chama cha soka cha England FA Gerrad ambaye pia ninahodha wa Liverpool amesema: "nimefurahia kila dakika niliyowakilisha nchi yangu na ni siku ya masikitiko kufahamu sitovaa tena jezi ya England."

Gerrard amekuwa na uzi wa England kwa miaka 14 ambapo ajafanikiwa kutwaa kombe lolote lile akiwa na katika jezi ya timu yake ya taifa huku akifanikiwa kuiwakilisha taifa lake kwenye makombe ya duni mara nne mwaka 2002, 2006, 2010 na 2014 ambapo alikuwa na hodha wa timu hiyo iliyo ishia katika hatua ya makundi.
Gerrard ameichezea England kwa miaka 14.

0 comments