
Wakazi wanatakiwa kukamata mbu wengi iwezekanavyo, wakiwa wazima au hata kama wamekufa, na mtu atakayekamata mbu wengi zaidi atapewa zawadi ya dola 100, imesema idara ya afya. Mshindi wa pili na wa tatu watapewa dawa ya kuzuia mbu na chandarua.
Watu wanatakiwa kuwatega mbu hao, au kuhifadhi 'mizoga' yao, kwa sababu itawasilishwa mbele ya maafisa kwa ajili ya kuhesabiwa.
Zaidi ya maambukizi 7,000 yameripotiwa mjini Kaohsuing, huku wagonjwa wapya mia mbili wakipatikana kila siku, limeripoti gazeti la China Post.
0 comments