Monday, 13 July 2015

AHADI YA KWANZA YA MAGUFULI HII HAPA

By    
Muda mfupi baada ya Dk John Magufuli kutangazwa na chama cha mapinduzi kupeperusha bendera ya chama hicho kugombea nafasi ya urais amewaahidi watanzania kuwa atahakikisha anawashughulikia wala rushwa na wabadhilifu wa mali za umma kikamilifu.

Ametoa ahadi hiyo katika viwanja vya jamuhuri mjini Dodoma alipokuwa anahutubia mkutano wa hadhara wakati chama chake kilipokuwa kinamtambulisha yeye pamoja na mgombea mwenza ambapo amesema pia atahakikisha wafanyabiashara ndogondogo wanafanyashughuli zao katika mazingira mazuri bila kubughudhiwa.

Kwa upande wake mgombea mwenza Mh Samia Hasan Suluhu amesema atahakikisha anashughulikia kero chache zinazoukabili muungano ili kuhakikisha unaimarika na unadumu.

Baadhi ya wakazi wa mji wa Dodoma wamepongeza uteuzi huo na kwamba CCM imefanya maamuzi sahihi kwani Dk Magufuli utendaji wake unafahamika na ni imani yao kuwa ana uwezo wa kuwatoa kwenye wimbi la umaskini.

0 comments