Monday, 13 July 2015

MUIGIZAJI WA VITIMBI AFARIKI NCHINI KENYA

By    
Muigizaji mashuhuri Afrika Mashariki kutoka nchini Kenya Benson Wanjau  maarufu kwa jina la "Mzee Ojwang" amefariki hii leo asubuhi katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta mjini Nairobi Kenya.

Katika uhai wake Mzee Ojwang alipata mashuhri katika michezo ya kuigiza ya kwenye luninga ya Tausi pamoja na Vitimbi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa katika ukurasa wa facrbook wa BBC Swahili Mzee Ojwang amefariki kutokana na ambukizo la ugonjwa wa pneumonia.

"Habari zinazotufikia zinasema kuwa Mzee Ojwang ameaga dunia kufuatia maambukizi ya pneumonia", ilieleza taarifa ya kwenye ukurasa wa BBC Swahili.

Msuni pamoja na timu nzima ya Aboodmsuni Network inawapa pole familia yake, familia ya uigizaji nchini Kenya kwa kumpoteza mtu muhimu katika familia yao.

Rest In Peace Mzee Ojwang

0 comments