Katibu mkuu wa chama ACT WAZALENDO, Samsoni Mwigamba akionyesha fomu ya kugombea nafasi ya urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha ACT WAZALENDO mara baada ya kupokea fomu hiyo katika ofisi za Tume ya uchaguzi (NEC) leo jijini Dar es Salaam. |
CHAMA Cha ACT-Wazalendo wamechukua fomu kwa ajili ya mgombea urais atakayepeperusha bendera katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam baada ya kuchukua fomu ya urais,Katibu Mkuu wa Chama hicho,Samson Mwigamba amesema kamati kuu imempitisha Profesa Kitila Mkumbo kuperusha bendera katika uchaguzi utaofanyika mwishoni mwa Oktoba mwaka huu.
Mwigamba amesema kuwa wamejipanga katika kushinda uchaguzi huo kutokana na watu waliokupwepo katika chama hicho ni wazalendo wa vitendo.
Amesema kuwa watu amesema chama chao ni kidogo lakini wameweza kusimamisha wagombea wa ,Udiwani,pamoja na ubunge ambapo katika vyama vyote vilivyoanizisha kwa kipindi kifupi vilishindwa kufanya hivyo.
Aidha amesema wanamuamini Profesa Mkumbo kutokana na malengo ya uanzishaji wa chama hicho kwa kutoa mchango mkubwa hivyo lengo la chama limetimia.
Amesema ambao wanahamia katika Chama hicho watapimwa uadilifu wao katika kuweza kuwatumikia wananchi wanao wachagua katika nafasi mbalimbali.
ACT-Wazalendo wamechukua fomu kwa kuwa idadi ndogo kuliko vyama vyote na utulivu ulitawala katika ofisi za tume ya Tifa ya Uchaguzi (NEC).
0 comments