Wednesday, 21 October 2015

SMZ YAIPONGEZA UN KWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA KIMAENDELEO VISIWANI ZANZIBAR

By    
IMG_9022
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo (kulia) na Mkuu wa ofisi ndogo ya Umoja wa Mataifa Zanzibar, Anna Senga (katikati) wakimkaribisha mmoja wa wageni waalikwa katika sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
SERIKALI ya mapinduzi Zanzibar imesema kuwa itaendelea kuthamini fursa mbali mbali zinazotolewa na Umoja wa Mataifa (UN) ili ziweze kuwanufaisha wananchi wote bila ya ubaguzi.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma, Haroun Ali Suleiman wakati akihutubia katika sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar, alisema umoja huo umekuwa sekta muhimu ya kuunga mkono juhudi za maendeleo ya serikali katika sekta mbali mbali za kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Alisema kuwa Zanzibar ikiwa miongozi mwa nchi zinazoendelea barani Afrika inaendelea kutumia vizuri fursa zinazotolewa na umoja huo kwa lengo la kujenga jamii bora zenye kipato na uwezo wa kati kwa lengo la kupunguza umasikini nchini.
Waziri Haroun alifahamisha kuwa miradi mbali mbali ya maendeleo inayotolewa na umoja huo imekuwa nyenzo muhimu ya kuisaidia serikali kuhudumia wananchi wake kwa ufanisi zaidi.
Alisema kutokana na misaada hiyo Zanzibar pia imekuwa mdau muhimu wa umoja huo kwani ni miongoni mwa nchi yenye urithi wa kimataifa kupitia maeneo ya Mji Mkongwe jambo ambalo ni ishara tosha ya mahusiano mema kati ya umoja huo na serikali.
IMG_9075
Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa visiwani Zanzibar wakibadilishana mawazo wakati wa kuwasili kwa wageni waalikwa kwenye sherehe hizo.
“ Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inajali kwa kiasi kikubwa juhudi za Umoja wa Mataifa kwa kutuunga mkono, nasi tunaendelea kutumia vizuri miradi mnayotuunga mkono.
Pia tunaendelea kukuombeni mtusaidie pale tutakapohitaji msaada wenu kwa Nyanja tofauti kwani bajeti ya serikali haitoshi kukidhi mahitaji yote ya kuendesha serikali.”, Alisema Waziri Haroun.
Naye Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alikiri kuridhishwa kwake na utekelezaji wa miradi mbali mbali ya umoja huo na kuahidi kuendelea kushirikiana vizuri na serikali ili kufikia dhana ya maendeleo endelevu Tanzania na Zanzibar kwa ujumla.
Bw. Rodriguez alibainisha kuwa umoja huo bado unaendelea kufanya tathimini na utafti juu ya masuala mbali ya kisiasa na kijamii nchini ili kuona ni kwa jinsi gani watasaidia kuunga mkono maeneo hayo kwa maendeleo ya nchi.
Alifafanua kuwa katika miradi mbali mbali iliyotekelezwa Zanzibar kupitia mashirika ya Umoja huo hasa UNDP, UN WOMEN na UNESCO miradi hiyo imeweza kufanikiwa zaidi ya asilimia 80 jambo ambalo ni faraja kwa umoja huo.
IMG_9170
Kila mtu alikuwa na tabasamu la furaha....Happy Birthday #UN70
Alieleza kuwa kupitia dhana ya maendeleo endelevu kwa mwaka 2016 umoja huo umejipanga kusaidia masuala mbali mbali ya haki za binadamu, utawala bora, uwazi na uwajibikaji, afya na vipaumbele vya kisera kwa serikali ili kuhakikisha Zanzibar inakuwa ni nchi ya kupigiwa mfano kimaendeleo.
“ Tuna kila sababu za kuishukru serikali ushiriki wake katika miradi yetu kwani bila wao kutuunga mkono vizuri leo hii tusingweza kuwepo hapa kusherekea mafanikio tuliyopata ndani ya miaka 70 ya UN hivyo nasi tunaahidi kuenzi mahusiano haya kwa lengo la kujenga jamii bora.”, alisema Bw.Rodriguez.
Aidha aliishauri serikali kuhakikisha mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu unafanyika kwa amani na kwa kuzingatia vigezo vya uwazi, uhuru na haki ili kila chama kilichoshiriki katika mchakato huo kinapata haki yake kwa mujibu wa sheria za nchi.
IMG_9044
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa ofisi ndogo ya Umoja wa Mataifa Zanzibar, Anna Senga.
“ Tunawatakieni uchaguzi mwema na wenye mafanikio bila ya kuwepo dalili za uvunjaji wa haki za binadamu ama kiashiria chochote cha vurugu ili muendelee kulinda heshima na mafanikio yaliyopatikana katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).” alisisitiza Bw. Rodriguez.
Sherehe hizo za kutimiza miaka 70 za UN zilifanyika katika ukumbi wa hoteli ya Serena Mjini Zanzibar na kuwashirikisha wadau mbali mbali wa umoja huo wakiwemo wawakilishi wa mashirika ya kimataifa yanayofanya kazi Zanzibar na kutoa Tuzo na vyeti vya kumbu kumbu kwa taasisi na shule zilizoshiriki kikamilifu katika utekelezaji wa baadhi ya miradi ya umoja huo.
IMG_9494
Ofisa anayeshughulikia masuala ya ushirikiano wa WHO Zanzibar, Dkt. Ghirmay Andemichael (kushoto) akibadilishana kadi na mmoja wa wageni waalikwa (ambaye jina lake halikuweza kupatikana kirahisi).
IMG_9166
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo (kushoto) akifurahi jambo na Mgeni rasmi Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma, Haroun Ali Suleiman.
IMG_9314
Mgeni rasmi Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma, Haroun Ali Suleiman (kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakizindua rasmi malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs) katika sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki.
IMG_9317
IMG_9327
Fataki zikipamba uzinduzi huo, sasa yamezinduliwa rasmi.
IMG_9368
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa katika sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja huo.
IMG_9352
Baadhi ya wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Dar na Zanzibar wakimsikiliza Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw.Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) wakati akitoa salamu za UN katika sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar.
IMG_9397
Mgeni rasmi Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma, Haroun Ali Suleiman akitoa salamu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar.
IMG_9407
Mgeni rasmi Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma, Haroun Ali Suleiman na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw.Alvaro Rodriguez pamoja na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakifanya 'Toast' katika kilele cha sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar.
IMG_9408
IMG_9418
'Toast' hiyo iliambatana na milipuko ya Fataki kusherehesha miaka 70 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake. Kwa picha zaidi bofya link hii

0 comments