Je wajua ya kwamba siku ya ijumaa kuna Saa ambalo mja hawezi akaliafiki saa hilo akiwa anaswali na kumuomba Allah isipokuwa Allah atampatia kile anacho kihitaji mja huyu?
Imesimuliwa na Abu Hurayra-Radhiya (r.a) Hakika Mtume (s.a.w) Alitaja siku ya ijumaa akasema "Ndani ya siku ya ijumaa kuna saa hawezi akaliafiki mja muislamu akiwa anaswali na kumuomba Mwenyezi Mungu chochote isipokuwa atapewa"
Mutafakun alayhi.
Na rai yenye nguvu juu ya saa hili: Ni kwamba saa hili lapatikana kati ya swala ya alaasiri na magharibi.
0 comments