Katika kipindi chake akiwa Old trafford amepata kufundisha vikosi vya aina tofauti, na huku akiwa na nyota wa aina tofauti katika vikosi vyake, ambapo Ryan Giggis ndiye mchezaji aliyekaa nae kwa mda mrefu zaidi.
Kama ilivyoada kuna kushuka na kupanda, sio kila siku itakuwa safi kwako, pamoja na hivyo united chini ya Ferguson haikutokea kuteteleka kwa sana na ndio maana amefanikiwa kutwaa mataji 33 yakiwa ni zaidi ya miaka aliyo ishi ndani ya Man united kama meneger.
Ugumu wa kuongoza benchi la ufundi unakuja katika mazingira ya kumtafuta mbadala wa mchezaji nyota pale anapo kosekana, kuanda mbinu mbadala endapo mbinu iliyo zoeleka kwa wachezaji wako itakambo shindwa kufanya kazi na mwisho ni kuunga timu kwa kuondoa matabaka na kuwafanya wachezaji kuwa chini yako na chini ya klabu.
Sir Alex Fergusano (Babu Fergi kama alivyozoeleka kuitwa katika vijiwe vyetu) kwa kiasi kikubwa aliweza kumudu changamoto za kuliongoza benchi la ufundi na kupelekea kuwa miongoni mwa mameneger bora ulimwenguni aliyepata kutokea.
Babu Fergi (mzee wa bigijii) alipata kufanya kazi na Catano ambapo alionekana kuwa muhimili wa timu hiyo na alipo ondoka babu aliziba pengo lake kwa kuibuka kwa David Beckahm ambapo timu ilibadili mfumo wa kumtegemea Catona na sasa kumzunguka Beckahm.
Katika hali ya kutaka kujiona ni bora zaidi ya klabu inasadikika ndio sababu ya Beckham kuondoka OT, na kuibuka kwa Vanestroy ambaye nae aliondoka na kuingia Cristian Ronaldo.
Kuondoka kwa Ronaldo mashabiki walikuwa na kiu ya kuona mbadala ama mfumo mpya utakao egemewa kwa mchezaji mwingi bila kuadhiri kiwango cha timu, ambapo napo alifanikiwa.
Huyo ndie Babu Fergi aliyefanya Man United kuwa na mashabiki wengi ulimwenguni, huku vijana wenye umri wa chini ya miaka 29 wakiwa na kiu ya kushuhudia united ya bila Mtafuna bigijii.
0 comments