Thursday, 9 May 2013

KILICHO ZUNGUMZWA NA HAKIM WAKATI WA HUKUMU YA SHEIKH PONDA KWA UFUPI

Kutoka katika blog ya Michuzi, Mahakamani Kisutu

[kwenye picha asikari wakiwa teyari kwa lolote mahakamami Kisutu, wakati hukumu ya Shekhe Ponda ikisomwa]

1. Mahakama hiyo haina uwezo wa kuzungumza mmilki halali wa kiwanja kutokana na masuala ya mgogoro ya ardhi kuwa na mahakama yake ingawa imegundua kuna tatizo katika umiliki.

2. Upande wa Serikali hakuwa na hoja ya kisheria wala ushahidi wa kutosha wa kuwatia hatiani watuhumiwa.

3. Hati ya Mashataka ilikuwa na mapungufu mengi ya kisheria.

4.Hakim awaonyesha njia ya kudai mali hiyo waisilamu kutokana na kile alichodai mali ya wakfu huwa haiuzwi wala haibadilishwi matumizi yaliyo kusudiwa

5. Upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kwamba watuhumiwa waliopo mbele ya mahakama ni wafuasi wa Shekhe Ponda.

Awasihi Waslamu kufuata taratibu za kisheria katika kudai haki yao

0 comments