Friday, 10 May 2013

WAISLAMU WAMCHANGIA PONDA NA WANATARAJI KUFANYA ITIKAFU

Waislamu waliojitokeza katika msikiti wa Mtambani hih leo wamepitisha mchango wa kumchangia Sheikh Issa Ponda, aliyewekwa katika kifungo cha nnje kwa mda wa mwaka mmoja.

[kwenye picha waislamu waliojitokeza katika msikiti wa Mtambani]

Mchango huo wa fedha ulichangishwa leo ni kwa ajili ya kwenda kufanya uchunguzi wa afya yake na kupata matibabu, baada ya kusota lupango (jela) kwa takribani miezi 7.

Shekhe Ponda na wenzake 49 walitolewa jela jana baada ya kutokutwa na hatia lakini Ponda akipewa kifungo cha nnje wakati wemzake wakiachiwa huru.

Wakati huo huo, uongozi wa Msikiti wa Mtambani umetangaza kufanyika itikafu ya kumshukuru Mungu kwa kukubali dua zao za huko nyuma, baada ya kuachiwa huru shekhe Ponda.

Itikaf hiyo itafanyika siku ya jumamosi ya mei 18 mwaka huu katika msikiti wa Mtambani na itaongozwa na shekhe Ponda

0 comments