Thursday, 24 October 2013

KORTINI KWA KUPIGA DEBE UBUNGO TERMINAL

WATU watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Jiji la Dar es Salaam wakikabiliwa na tuhuma za kupiga debe eneo lisiloruhusiwa la Ubungo Terminal.

Watuhumiwa hao ni Fredy Laurence (30) mkazi wa Ubungo, Godfrey Magasha(17), mkazi wa Mbagala na Elisi Rahilo (23), mkazi wa Tabata.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Timothy Lyon, Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Richard Magodi, alidai Oktoba 23, mwaka huu, washitakiwa hao walikamatwa wakipiga debe stendi ya mabasi ya Ubungo na kuwalazimisha abiria wapande kwenye magari ya abiria.

Kesi imeahirishwa hadi Novemba 5, mwaka huu na washitakiwa wamerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo ni kuwa na wadhamini wawili wenye vitambulisho na barua ya Serikali za Mitaa, watakaosaini bondi ya sh 100,000 kila mmoja.


CHANZO: TANZANIA DAIMA

0 comments