Wednesday, 23 October 2013

MITAMBO YA RUVU CHINI KUZIMWAWA JUMAMOSI, MAENEO KADHAA DAR KUKOSA MAJI

SHIRIKA LA MAJI SAFI NA MAJITAKA DAR-ES-SALAAM (DAWASCO), LINAWATANGAZIA WAKAZI WA JIJI LA DAR-ES-SALAAM NA MJI WA BAGAMOYO MKOANI PWANI KUWA, MTAMBO WA KUZALISHA MAJI RUVU CHINI UTAZIMWA KWA WASTANI WA SAA 12 SIKU YA JUMAMOSI, TAREHE 26/10/2013, KUANZIA SAA 01:00 ASUBUHI HADI 01:00 USIKU.

MTAMBO WA RUVU CHINI UTAZIMWA ILI KURUHUSU MKANDARASI KUFANYA KAZI YA KUUNGANISHA BOMBA LINALOTUMIKA LA MAJI GHAFI (RAW WATER) NA BOMBA JIPYA KARIBU NA MABIRIKA (CLARIFIERS) NDANI YA MTAMBO.

KWASABABU HIYO MAENEO YAFUATAYO YATAKOSA MAJI:

MJI WA BAGAMOYO, VIJIJI VYA MAPINGA, KEREGE NA MAPUNGA. BUNJU, BOKO, TEGETA, KUNDUCHI, SALASALA, JANGWANI, MBEZI BEACH NA KAWE.

MAENEO MENGINE NI MLALAKUWA, MWENGE, MIKOCHENI, MSASANI, SINZA, MANZESE, MABIBO, KIJITONYAMA, KINONDONI, OYSTERBAY, MAGOMENI, UPANGA, KARIAKOO, CITY CENTRE, ILALA, UBUNGO MAZIWA, KIGOGO, MBURAHATI, HOSPITALI YA RUFAA MUHIMBILI, BUGURUNI, CHANGOMBE NA KEKO.

WANANCHI MNASHAURIWA KUHIFADHI MAJI NA KUYATUMIA KWA MATUMIZI YA LAZIMA.

DAWASCO INAWAOMBA RADHI KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU
“DAWASCO TUTAKUFIKIA”

0 comments