Uingereza imeaanza kutafiti wa kuanzishwa kwa mfumo wa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya nchi hiyo
itakayoendana na kanuni na mfumo wa fedha na uchumi wa kiislamu.
Waziri wa Sayansi na elimu ya juu David Willetts alitangaza mpango huo wakati alipokuwa akitoa hotuba jijini London Alhamis.
Mapendekezo ya mfumo huo yatawapa fursa wanafunzi wa kiislamu ambao wamekuwa wakiikwepa kutokana na riba iliyokuwemo kwenye mikopo hiyo.
Akizungumza katika mkutano wa vyuo vikuu vya Uingereza Waziri David Willetts alisema sheria hiyo ya kiislamu itatoa fursa zaidi ya upatikanaji wa wanafunzi wenye vipaji na ujuzi kuliko mfumo sasa unaowanyima baadhi ya wanafunzi wa kiislamu kukwepa mikopo hiyo.
Mapendekezo ya mfumo huo tayari yamefunguliwa kwa kila mwenye ushauri wa namna ya uendeshwaji ameruhusiwa kufanya hivyo.
Hii si ajabu kwa nchi ya Uingereza kuwa na mfumo wa fedha unaoendeshwa kwa sheria za kiislamu. Baadhi ya mabenki yamekuwa yakiendeshwa kwa taratibu za Uchumi wa kiislamu ikiwemo benki ya serikali ya Uingereza ya IBB (islamic bank of britain).
Mwaka jana Waziri Mkuu wa uingereza David Cameron akizungumza katika kongamano la uchumi la World Islamic jijni London alisema anataka kuifanya London kuwa kituo kikuu cha uchumi wa kiislamu duniani.

0 comments